KIPENGELE cha Rasimu ya
Katiba kinapendekeza
uwepo wa Serikali tatu, ya
Muungano, ya Mapinduzi
Zanzibar na Tanzania Bara,
kimezidi kupingwa ambapo
safari hii, kipengele hicho
kimedaiwa kisipoondolewa
kitaathiri sekta ya anga.
Mtaalamu na Mshauri wa
masuala ya anga nchini,
Mtesigwa Maugo, amesema
sekta hiyo itaathirika kwa
kuwa katika mambo saba
yanayoshughulikiwa na
Serikali ya Muungano, sekta
ya anga haipo.
Maugo, ambaye amewahi
kuwa Mkurugenzi Mtendaji
Mwanzilishi wa Taasisi ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki
inayoshughulikia usimamizi
wa usalama wa Usafiri wa
Anga (CASSOA), alisema hayo
jana katika ofisi za gazeti hili,
Dar es Salaam.
“Mfumo wa kimataifa wa
usafiri wa anga una
changamoto ambazo
zinatakiwa ziangaliwe
wakati huu ambapo rasimu
hii inajadiliwa, lengo hasa ni
kujiaminisha kama kuna
mantiki kwa sekta hii
kuiweka moja kwa moja
katika majukumu ya Serikali
ya washirika,” alisema
Maugo.
Alisema usimamizi wa usafiri
wa anga na biashara ya
usafiri huo kati ya mataifa ni
suala linalotakiwa kuwa
chini ya nchi, uratibu wa
sekta hiyo unaendeshwa na
Shirika la Kimataifa la Usafiti
wa Anga (ICAO) ambalo liko
chini ya taasisi ya Umoja wa
Mataifa inayoshughulikia
usafiri wa anga.
Alisema pia masuala ya
uanachama wa shirika la
kimataifa la usafiri wa anga,
usajili wa ndege, usimamizi
wa kampuni za ndege,
usimamizi wa masuala ya
usalama, biashara ya ndege
na nchi za nje na huduma za
uongozaji ndege na udhibiti
wa anga yote yanahitaji
kuwa chini ya nchi moja
husika.
Alisema katika baadhi ya
masuala hayo kunahitaji
umuhimu wa nchi husika
kuwa mwanachama wa
shirika la ICAO, pia suala la
usafiri wa ndege itabidi kila
nchi iwe na alama yake ya
utambulisho na daftari lake
badala ya sasa ya 5H.
“Pia katika eneo la usimamizi
wa kampuni za ndege
mkataba wa kimataifa wa
usafiri wa anga unataka nchi
inayosimamia shirika au
kampuni lazima ipewe cheti
maalumu kinachoruhusu
kutoa huduma hiyo,
marubani na wahudumu
nao wapatiwe leseni, sasa
kwa kuondoa sekta hii
kwenye muungano kila nchi
itatakiwa isimamie masuala
haya yenyewe,” alisema.
Aidha alisema kwa mujibu
wa taratibu hizo za usafiri
wa anga nchi husika
inatakiwa kuwa na taasisi
itakayosimamia masuala ya
usafiri wa anga ambayo
itawakilisha nchi husika
katika ICAO.
“Ni gharama kubwa
kuendesha taasisi hii lakini
kwa rasimu hii ya Serikali
tatu itabidi kila nchi iwe na
taasisi yake.”
Alisema kipengele hicho cha
serikali tatu kinaacha
mashaka kwa kuwa pamoja
kwa kwamba hautajwi
uhusiano wa kimataifa,
lakini ruhusa hiyo ya Katiba
inatosha kuleta vurugu na
kuvunja utaifa.
“Kuna baadhi ya mashirika
ya kimataifa kigezo cha
kujiunga nayo ni taifa huru,
je, hii itakuwaje kwa sekta
hii.”
Alipendekeza ili kulinda
utaifa wa Tanzania mambo
yanayoshughulikiwa na
Serikali ya Muungano ni
vyema yakaangaliwa kwa
makini kuliko kuyapunguza
ambapo pia alishauri
mjadala wa rasimu kuhusu
kipengele hicho ujikite
katika kutatua matatizo ya
watanzania na si kuangalia
idadi ya Serikali.
No comments:
Post a Comment