Wednesday, August 14, 2013

MWANAFUNZI ATEKWA HUKO MOSHI NA KUFANYISHWA NGONO KWA SIKU NNE

MWANAFUNZI wa kidato cha
kwanza katika shule ya
sekondari Marangu
inayomilikiwa na kanisa Katoliki
jimbo la Moshi, (jina
limehifadhiwa) alitekwa na
kukufungiwa kwenye hoteli
moja ya kitalii mjini hapa na
kufanyiwa vitendo vya ngono
kwa muda wa siku nne
mfululizo.
Mwanafunzi huyo anadaiwa
kutekwa Agosti 6 mwaka huu
na kijana mmoja (jina
linahifadhiwa) mfanyakazi wa
kampuni ya simu za mikononi
(Airtel) mjini Dodoma.
Akizungumza jana na Tanzania
Daima Jumatano, kaka wa
mwanafunzi huyo, Joseph
Temba, alidai mdogo wake
alitekwa na mtu huyo na tayari
mtuhumiwa ameshakamatwa.
Alisema walifanikiwa
kumkamata mtuhumiwa huyo
Agosti 10, mwaka huu, katika
baa moja akiwa na mdogo
wake baada ya raia wema
kutoa taarifa za kuonekana
kwake.
Kwa mujibu wa kaka wa
mwanfunzi huyo siku ya tukio
alipokea simu kutoka kwa
mwangalizi wa wanafunzi
(matroni) akimjulisha
kutokuwapo bwenini kwa
mdogo wake na ndipo
walipoanza kufuatilia na kutoa
taarifa kituo kikuu cha polisi
mjini Moshi na kupewa namba
Mos/RB/9196/2013.
Alisema siku iliyofuata ya Agosti
saba jioni walipokea simu
kutoka kwa watu wa karibu
wakiwataarifu kuwapo katika
hoteli hiyo mdogo wake lakini
baada ya kufika walinyimwa
kuona kitabu cha wageni ili
kuangalia orodha ya majina ya
wageni waliofikia hapo ili
kujiridhisha kama mtuhumiwa
huyo alikuwapo mahali hapo.
Hata hivyo alisema jioni ya
Agosti 10 walipokea taarifa za
kuonekana kwenye baa hiyo
mtuhumiwa akiwa na mdogo
wake na kuwajulisha polisi na
hatimaye kufanikiwa kumtia
mbaroni ambapo hadi sasa
bado anahojiwa na jeshi la
polisi.
Chanzo cha kutekwa kwa
mwanafunzi huyo ni
mawasiliano ya simu baina ya
mtekaji na mwanafunzi huyo
ambapo inadaiwa mtuhumiwa
huyo alimrubuni mwafunzi
huyo kuacha masomo na
kwamba angemtafutia nafasi
kwenye shule kubwa za
kimataifa.
Inadaiwa kwamba mwanfunzi
huyo alikubaliana na
propaganda hiyo na kutoka
shuleni jioni ya Agosti 6 na
kumfuata mtuhumiwa kwenye
gari lake na kwenda naye hadi
Moshi mjini umbali wa kilomteta
50 kutoka shule ya sekondari
Marangu.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Kilimanjaro, Robert Boaz,
alisema hana taarifa za kutekwa
kwa mwanafunzi huyo kwa kile
alichodai alikuwa ametingwa na
majukumu ya kikazi mjini
Arusha na kuahidi kulifuatilia
baadaye.
Tanzania daima

No comments:

Post a Comment