Wednesday, August 14, 2013

JAJI MKUU MSTAAFU KUTOA USHAHIDI JARIBIO LA KUMTAPELI WILLBROD SLAA

Hai. Jaji Mkuu Mstaafu,Barnabas
Samatta ni miongoni mwa
mashahidi 12 watakaotoa
ushahidi katika kesi ya jinai ya
jaribio la kumtapeli Katibu Mkuu
wa Chadema,Dk Willbrod Slaa.
Wengine watakaotoa ushahidi
katika kesi hiyo inayomkabili
Abedi Adam Abedi (22) ni Dk Slaa
mwenyewe na Mbunge wa
Arusha Mjini kwa tiketi ya
Chadema, Godbless Lema.
Orodha ya majina ya mashahidi
hao ilitolewa mahakamani juzi
mbele ya Hakimu Mkazi wa
Wilaya ya Hai, Denis Mpelembwa
na Mwendesha Mashtaka wa
Takukuru, Maghela Ndimbo.
Wengine watakaotoa ushahidi ni
wakili mashuhuri wa Chadema,
Profesa Abdalah Safari, Rumisha
Slaa, Happynes Masue, Godfrid
Njau, Gervas Geneya, Neema
Godbless,Aron Misanga, Prosper
Mbilinyi na Judith Mashashi.
Akisoma maelezo ya awali,
Ndimbo alidai kuwa kati ya Aprili
na Mei, 2012, mshtakiwa
alijitambulisha kwa Dk Slaa, Lema
na Profesa Safari kuwa yeye ni
mtumishi wa Takukuru.
Ilidaiwa kuwa katika kipindi
hicho, mshtakiwa aliwapigia
simu Dk Slaa, Lema na Profesa
Safari na kujitambulisha kuwa
yeye ni Abel Kibaso Mkuu wa
Takukuru Wilaya ya Ulanga.
Katika kipindi hicho pia,
mshtakiwa aliwapigia simu
viongozi hao akijitambulisha ni
Jaji mstaafu Samatta akitaka
wampe pesa ili washinde katika
kesi iliyokuwa mahakama ya
Rufaa.
Rufaa hiyo namba 47/2012
ilifunguliwa na Lema dhidi ya
Mussa Hamisi na wenzake
akipinga hukumu ya Mahakama
Kuu Arusha ya kupinga kuvuliwa
Ubunge wa Arusha mjini kesi
ambayo kwa sasa ilishatolewa
uamuzi.
mashtaka huyo alidai
mahakamani kuwa mshtakiwa
alijifanya ni Jaji Mkuu Mstaafu
Samatta wakati akijua siyo Jaji
Samatta kwa lengo tu la kujipatia
fedha kinyume cha sheria.
Hata hivyo Lema alishinda Rufaa
hiyo na kurudishiwa Ubunge
wake.
Mshtakiwa amekanusha
mashtaka hayo na kesi hiyo
imepangwa kuanza kusikilizwa
rasmi Septemba 25 ambapo Jaji
Samatta ni miongoni mwa
mashahidi wa upande wa
Jamhuri.

No comments:

Post a Comment