Wednesday, August 14, 2013

SHILOLE ASHUSHIWA KIPIGO KISA MADENI.....

Msanii nyota kwenye tasinia ya
muziki na filamu bongo Zuwena
Mohamed “ Shilole” mwishoni
mwa wiki iliyopita alionja joto
ya jiwe baada ya kutiwa mtu
kati na wakina dada waliokuwa
wanamdai kiasi kikubwa cha
pesa.
Habari za uhakika
zilizothibitishwa na mmoja wa
wakina dada hao waliokuwa
wanamdai zilisema kuwa
wanawake hao waliamua
kuchukua hatua za kumtia
adabu Shilole baada ya kupata
taarifa kuwa siku hiyo alikuwa
ana hama kwa kukimbia na teni
lao “ Ishu ilikuwa hivi sisi
tunamdai huyu dada lakini cha
kushangaza amekuwa
akitupiga chenga sana na ona
alivyokuwa sio mstaarabu
kumbe siku hiyo alikuwa
anahama na deni letu ndio
maana tuliamua kwenda
kumzingua” Alisema dada huyo
aliomba jina lake lihifadhiwe.
Dada huyo aliendelea
kufunguka mengi kuhusu
sakata hilo “ Unajua sisi
tunafanya biashara zetu hivyo
kuna siku Shillole alikuja na
kusema amekwama kipesa
hivyo tumuazime pesa na
tukafanya hivyo lakini cha
kushangaza mwezi wa sita huu
hataki kurudisha na amekuwa
akitukwepa mara kwa mara
hivyo majirani ndio
wakatushtua kuwa anataka
kuhama kwa staili ya kutoroka
na deni letu ndipo tulipoenda
wanawake wanne na
kumshushia kipigo” Alisema
dada huyo
Baada ya taarifa hizo Shilole
alitafutwa kupita simu yake ya
mkononi pamoja na kupita
kwenye makoloni yake
hakuweza kupatikani
isipokuwa majirani mbalimbali
walikili kutokea kwa tukio hilo
la kufedhehesha kwa msanii
huyo.

No comments:

Post a Comment