Thursday, August 8, 2013

PONDA KUUNGURUMA IDD PILI

WAKATI Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar (SMZ) ikimpiga
marufuku Katibu wa Jumuiya
ya Kiislamu Nchini, Shekhe
Ponda Issa Ponda,
kuendesha mihadhara ya
kidini katika ardhi ya
Zanzibar yenye mwelekeo
wa kuleta mifarakano na
uhasama kwa jamii, Umoja
wa Wahadhiri wa dini ya
Kiislamu Mkoa, umemwalika
kuongoza kongamano la
Baraza la Iddi.
Kongamano hilo
limepangwa kufanyika siku
ya Iddi Pili kwenye viwanja
vya shule ya msingi Kiwanja
cha Ndege mjini hapa.
Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi ya kongamano
hilo, Idd Msema, alisema
hayo jana mbele ya
waandishi wa habari kuwa
Jeshi la Polisi limekubali
kufanyika kwa kongamano
hilo.
Kwa mujibu wa Msema,
Polisi imetoa masharti
kwamba yasitumike maneno
ya kashfa dhidi ya dini
zingine au kiongozi wa
Serikali kwa kutumia vipaza
sauti au sauti ya kawaida.
Barua ya Polisi ya kuruhusu
kufanyika kongamano hilo,
imenukuu kifungu namba
43 (1) na 44 ambacho
kinalipa mamlaka Jeshi hilo
kusimamisha mara moja
mkutano kama huo mara
itakapobainika kuwapo hali
ya vurugu inayotishia amani
na usalama.
Hata hivyo, alisema
madhumuni ya kongamano
hilo ni kukumbusha
Waislamu masuala muhimu
yahusuyo dini yao, hasa
baada ya kutoka katika
Mfungo wa Mwezi Mtukufu
wa Ramadhan.
Kwa mujibu wa Msema,
kongamano hilo
litashirikisha mashekhe wa
wilaya zote za mkoa wa
Morogoro, waumini wa dini
ya kiislamu na wasiokuwa
waumini wa dini hiyo.
Pia alisema litajikita kujadili
maisha baada ya Mfungo
ambapo mashekhe pamoja
na Ponda watatoa mhadhara
huo. Katibu wa Maandalizi ya
Kongamano hilo, Nassoro
Abdallah Nassoro, alisema
wanatarajia umati mkubwa
wa waumini na watu
wengine watajitokeza katika
kutokana na uwepo wa
Shekhe Ponda.
Shekhe Ponda hivi karibuni
alihukumiwa kifungo cha nje
cha mwaka mmoja baada ya
Mahakama kumkuta na hatia
ya mashitaka aliyofunguliwa
ya kuingilia kiwanja
kilichoko Chang’ombe
Markazi, kinachomilikiwa na
kampuni ya Agritanza.
Habari leo

No comments:

Post a Comment