Nakuru. Katika hali isiyo ya
kawaida wanandugu watano
kutoka familia moja wamefunga
ndoa siku moja nchini Kenya.
Tukio hilo lililoibua mshangao
miongoni mwa watu
walioshuhudia lilitokea katika
kanisa la mtakatifu Peter mjini
Nakuru.
Maharusi waliojawa na furaha
isiyo na kifani walielezea kuwa
malezi yao bora yaliwafanya
wote kuchagua kufunga ndoa
siku moja.
Samson Wachira, ambaye ni wa
kwanza kuzaliwa alisema wazazi
wao waliwaonyesha kupendana
na kushirikiana katika mambo
yote tangu wakiwa wadogo hali
iliyowapelekea kukua katika
mazingira hayo.
Hivyo basi, Wachira alielezea
kuwa kila mmoja wao alipotaka
kufunga ndoa rasmi, aliwaita
nduguze kwa ushauri.
Wachira ana mika 36 ilhali
George Wango, ambaye ni wa
mwisho kuzaliwa ana umri wa
miaka 24.
Wengine walikuwa Peter
Mbugua, 35, Stephen Kinyanjui,
34, na Harman Kago,32.
Ndugu hao waliitaja siku hiyo
kama ya furaha ambayo
walikuwa wakiingojea kwa
hamu kubwa kutokana na
kufikia kupiga hatua moja
maishani mwao .
“Tumekuwa tukiingoja na
kujitayarisha kwa siku hii kwa
mwezi mmoja uliopita,” alisema
Wango, mmoja wa maharusi hao
Wazo la kufunga ndoa siku moja
liliwajia ndugu hao miezi saba
iliyopita wakati kasisi mmoja
alipowatembelea nyumbani
kwao eneo la Kiratina.
Baba yao aliandaa karamu na
ibada ya misa ya shukrani wakati
kasisi alitaka kujua ni nani kwa
familia hiyo alikuwa
amekubaliwa kupokea
sakramenti.
Kulingana na desturi za kanisa la
Katoliki, ni sharti mwanamume
awe amefunga ndoa rasmi
kanisani ili kuruhusiwa kupokea
sakramenti hivyo kasisi huyo
aliwapa changamoto vijana hao
kuhusu faida za kufunga ndoa
kanisani.
No comments:
Post a Comment