AFYA:- MBEGU ZA
MABOGA: ZINA UWEZO WA
KUKUEPUSHA NA
MAGONJWA 10 HATARI~-
PERUZI KUYAFAHAMU
~MBEGU ZA MABOGA: ZINA
UWEZO WA KUKUEPUSHA NA
MAGONJWA 10 HATARI~~~
A/Alleykum;
ZIKIWA zimesheheni protini na
madini kadhaa kama vile
chuma, kopa, maginizia,
manganizi na zinki, mbegu za
maboga zinakuwa mbegu bora
na muhimu kutafuna kila wakati
kama wewe ni mpenzi wa
kutafuna-tafuna. Imethibitika
pasipo na shaka kuwa mbegu
za maboga zina faida lukuki
kiafya na zina uwezo wa
kukuepusha na magonjwa
hatari zaidi ya 10:
UGONJWA WA MOYO:
Mbegu za maboga zina kiasi
kingi cha madini aina ya
maginizia (magnesium) ambayo
huboresha utendaji kazi wa
viungo vya mwili. Huimarisha
usukumaji wa damu kwenye
moyo, huimarisha ukuaji wa
mifupa na meno, huifanya
mishipa ya damu kupitisha
damu kwa urahisi na hufanya
upatikanaji wa haja kubwa
kuwa laini.
KINGA YA MWILI:
Mbegu za maboga pia zina kiasi
kingi cha madini ya Zinki (Zinc).
Madini haya yana faida nyingi
mwilini, ikiwemo kuimarisha
kinga ya mwili, kuboresha
ukuaji na uundaji wa
chembechembe hai za mwili,
kuboresha usingizi, kuboresha
ladha mdomoni na harufu,
huboresha afya ya macho na
ngozi, hurekebisha sukari na
huboresha nguvu za kiume pia.
Upungufu wa madini ya ‘Zinc’
mwilini una uhusiano mkubwa
sana na matatizo ya kuzaa
watoto njiti, kuota chunusi
nyingi mwilini, watoto kuwa na
uwezo mdogo darasani
kimasomo na matatizo mengine
mengi ya kimwili na kiakili.
MAFUTA YA OMEGA -3:
Omega-3 ni moja kati ya mafuta
muhimu sana mwilini. Jamii ya
karanga pamoja na mbegu za
maboga ni miongoni mwa
mbegu zenye kiasi kingi cha
mafuta aina hii. Hivyo ulaji wa
mbegu za maboga
utakuwezesha kupata
kirutubisho hiki muhimu katika
mwili wako na kukupa faida za
mafuta haya ambazo ni nyingi.
KIBOFU CHA MKOJO:
Tangu enzi za mababu zetu,
mbegu za maboga zimetumika
kuimarisha afya ya wanaume
kutokana na kuwa na kiasi
kingi sana cha madini aina ya
Zinc ambayo ni muhimu sana
kwa afya ya kibofu cha mkojo.
Mbegu za maboga pamoja na
mafuta yake, yote kwa pamoja
hutoa kinga kwenye kibofu
kupatwa na matatizo ya kiafya,
yakiwemo yale ya saratani ya
kibofu.
KINGA DHIDI YA SARATANI:
Imethibitika kwamba watu
ambao hula mlo wenye kiasi
kingi cha mbegu za maboga
wamegundulika kuwa na hatari
ndogo sana ya kupatwa na
saratani za tumbo, matiti,
mapafu na kibofu.
UGONJWA WA KISUKARI:
Utafiti uliofanywa kwa
kuwalisha wanyama mbegu za
maboga, umeonesha kuwa ulaji
wa mbegu za maboga, husaidia
kurekebisha kiwango cha
‘Insulin’ mwilini na hivyo
kumuepusha mtu kupatwa na
ugonjwa wa kisukari.
MATATIZO YA UKOMO WA HEDHI:
Mara nyingi kina mama watu
wazima ambao wamefikia
ukomo wa hedhi, hupatwa na
matatizo mbalimbali
yanayosababishwa na hali hiyo.
Hata hivyo utafiti umeonesha
kuwa mbegu za maboga zina
uwezo wa kurekebisha hali hiyo
na kuondoa kabisa matatizo ya
kiafya yatokanayo na ukomo wa
hedhi.
AFYA YA MOYO NA MAINI:
Mbegu za maboga, ambazo zina
kiasi kingi cha mafuta mazuri,
kamba lishe na virutubisho
vinavyoimarisha kinga ya mwili
(antioxidants), zimeonekana
kuwa bora pia kwa afya ya
moyo na ini, huweza kumpatia
mlaji kinga dhidi ya matatizo ya
kiafya katika moyo na ini.
DAWA YA USINGIZI:
Mbegu za maboga
zimegundulika pia kuwa na
kirutubisho kinachozalisha
‘homoni’ za usingizi. Ulaji wa
mbegu za maboga saa chache
kabla ya kupanda kitandani,
hasa ukila pamoja na tunda
lolote, kunasaidia kupata
usingizi mzuri na tulivu.
DAWA YA UVIMBE:
Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa
mbegu za maboga zina mafuta
yenye uwezo wa kutoa kinga
dhidi ya magonjwa ya uvimbe
(inflamatory diseases) sawa na
dawa aina ya ‘indomethacin’,
lakini mbegu hizi hazina
madhara kama ilivyo kwa hiyo
dawa.
JINSI YA KULA MBEGU ZA
MABOGA
Ili kupata faida zake zote,
zikiwemo zile za mafuta yake,
inashauriwa kula mbegu hizo
zikiwa kavu, bila kuzikaanga.
Hakikisha pia unapata mbegu
zilizohifadhiwa vizuri ambazo
hazijaoza wala kuwa na fangasi.
Iwapo utapenda kuzikaanga,
basi hakikisha unazikaanga
kwa muda usiozidi dakika 15,
unaweza pia kuongeza chumvi
kidogo kupata ladha, lakini za
kukaanga zitakuwa hazina
mafuta mengi kama zile kavu.
...........Wabillahy towfiq...............
No comments:
Post a Comment