Mahsusi kwa watu wanaotarajia
kuanzisha mahusiano thabiti na
yenye malengo, pamoja na wale
ambao tayari wamo ndani ya
mahusiano ya aina hiyo.
KWA WATARAJIA
1. Usidanganyike na
muonekano wa nje au yale
maongezi ya Mwanzo
Kila mtu huwa mstaarabu siku
za mwanzo hata wale ambao
sio.
2. Usikimbilie kutangaza nia
haraka
Siku zote ni rahisi mtu kuwa
muwazi kwa rafiki yake kuliko
kwa mtu ambae anajua anataka
mahusiano nae kwa hofu ya
kumpoteza. Tumieni muda
wakutosha kufahamiana kama
marafiki kabla hamjajiingiza
kwenye uhusiano wa kimapenzi.
3. Uliza maswali kuhusu vitu
ambavyo ni muhimu sana
kwako
Kwa mfano kama ni mtu wa
familia au sio taka kujua
mawazo yake kuhusu watoto hii
itaepusha migongano isiyo ya
lazima hapo baadae.
4. Penda kujua malengo yake
ya Baadae
Hii itakuwezesha kugundua ni
mtu wa aina gani......kama ni
mpenda maendeleo, mtu wa
starehe tu n.k
5. Kuwa Muwazi
Hii inakwenda kwa pande zote,
kuna vitu ambavyo ukimwambia
mtu ni vidogo sana ila ukificha
vinakua, kwavile tu ulifanya siri.
6. Hakikisha uwezo wenu wa
kuelewa unaendana
Hapa siongelei darasa ila
mnavyokuwa sambamba
kwenye maongezi ya kawaida tu
yasiyohitaji degree.
7. Onyesha Misimamo yako
hata kama unaona ni migumu
kueleweka
Ni vizuri mtu akikubali/taka
kujiingiza kwenye mahusiano na
wewe awe akijua atakua na mtu
wa aina gani. Kama hupendi
nguo fupi, mwanamke/
mwanaume mnywaji pombe,
mvuta sigara n.k, sio unasubiri
mpaka muwe pamoja ndo
muanze kuzozana.
8. Hakikisha kuna vitu
mnavyoshabihiana
Ni muhimu mkiwa na vitu
mnavyoweza kufanya
pamoja........iwe ni kuangalia
movie ama kutembea nyakati za
jioni inasaidia kuimarisha
ukaribu wenu kuliko kila mtu
kwenda na njia zake.
KWA WALIO NDANI YA
MAHUSIANO
1. Mheshimu Mwenzako
Heshima ni kitu kidogo sana
kutoa ila kikubwa kwa
anaepokea...kuwa muangalifu
unavyomwongelesha na
kumfanyia mwenzako pindi
muwapo na watu wengine
2. Kuwa muelewa na
mvumilivu
Kama mlikuwa mmepanga ama
kuahidiana kitu fulani halafu
hakijafanyika usianze kwa
lawama.........ohh
hunipendi........mara hunijali.
Omba sababu na ukipewa elewa
kama hakikufanyika leo
kitafanyika kesho..........dunia
haikimbii.
3. Msome mwenzako
Ukijua tabia za mtu ni rahisi
sana kumuelewa na kukidhi
mahitaji yake. Kama ukijua
mwenzi wako anahitaji nini
pindi anapokasirika....nafasi ya
kutuliza hasira ama
kubembelezwa papo hapo
itasaidia kutokuongezeana
hasira kwa kumfanyia kile
ambacho sicho anachohitaji.
4. Kuwa mwepesi wa kuomba
msamaha
Usipende
kujikweza.......kujishusha kidogo
kwenye mahusiano haimaanishi
wewe ni duni.
5. Kuwa msikilizaji zaidi ya
Muongeaji
Kuna wakati mwenzi wako
anakuwa anahitaji kutoa
yaliyomo moyoni mwake
tu.....iwe hasira ama furaha bila
kuingiliwa na ushabiki ama
upinzani kwahiyo soma alama
za nyakati.
6. Onyesha kujali
Wakati mzuri kumwonyesha
unamjali ni pale anapokuwa na
wakati mgumu.....iwe ni
kifedha......kiafya.....kikazi na
mengineyo, sio lazima umpe
pesa kama ndicho
anachohitaji....ama kumpiga
ngumi kama ni swala la ugomvi,
maneno mazuri ya
faraja....kumuonyesha uko
pamoja nae na kwamba
unaumia anapoumia yeye,
inatosha kabisa kumpa
mwenzako ahueni.
7. Kuwa msiri
Jiheshimu wewe pamoja na
mwenzi wako,matatizo yenu
ndani sio yakuanika nje kila
anaepita aone. Inapotokea
mmekosana sio mwenzako
akitoka tu kwa hasira na wewe
unachukua simu ama mguu
huyo mpaka kwa shoga na
shangazi wote wajue leo kwako
kuna ugomvi. Na sio hata
mambo madogo tu, utake
msuluishwe na mtu wa
nje....malizeni humo humo ndani.
8. Wivu
Wivu ni mzuri katika
kupendezesha mahusiano ila, ni
zaidi ya kero pale unapozidi.
Kuwa na kiasi.........
9. Mpe nafasi yake
Kuwa pamoja ndani ya
mahusiano haina maana
mfuatane pamoja kila upande
wa jiji.....kumbuka yeye ana
marafiki na wewe una wako sio
kila unachofanya lazima na yeye
afanye!
10. Imani
Iwapo mtu hajakupa sababu ya
kutokumuamini.........muamini.
Inakera sana pale mtu
anapoonyesha wasiwasi na
wewe iwapo hujafanya
chochote kusababisha hilo. Pia
jiamini wewe mwenyewe kama
wewe........unapendwa.........wewe
unathaminiwa.......wewe sio hata
salamu tu ikitolewa kwa
mwingine unaanza kuwaka.
11. Kuwa mkarimu
Kuwa mkarimu kwa ndugu na
marafiki wa Mwenzi wako. Sio
lazima mdogo wake umlipie Ada
wewe...ama umpelekee mama
yake gunia la mchele, kitendo
cha wewe kumsukuma kufanya
hivyo iwapo atakua anajiuliza
afanye au inatosha kuonyesha
upo upande gani.
12. Usiwe na kiburi
Kiburi hakijawahi kujenga
popote. Kununa kwa muda
mfupi kunaeleweka na
kunakubalika iwapo
umekorofishwa. Ila kususa
chakula.......kuhamishana
chumbani na kunyimana
unyumba havijengi bali
vinabomoa . Ndo mwanzo wa
kutafutiwa msaidizi.
13. Mwisho kabisa, usisahau
KUSHUKURU na KUTOA SIFA kila
mara
Kumsifia na kumshukuru
mwenzi wako kila mara
itamfanya ajihisi anapendwa na
itamfanya afurahie kuwa karibu
na wewe tofauti na mtu ambae
anatoa malalamiko tu.
No comments:
Post a Comment